Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 10

Mfano wa Msamaria mwema

25 Wakati huo mtaalamu mmoja wa Torati alisimama ili kumjaribu Isa, akamuuliza, "Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?"

26 Isa akamjibu, "Imeandikwaje katika Torati? Kwani unasoma nini humo?"

27 Akajibu, " Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; tena, Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ "

28 Isa akamwambia, "Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também