40 Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike. Martha akaja kwa Isa na kumuuliza, "Bwana, hujali kwamba dada yangu ameniachia kazi zote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie."
41 Lakini Bwana Isa akamjibu, "Martha, Martha, mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? 42 Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Mariamu amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea."