Tubu au utaangamia
1 Wakati huo huo, kulikuwa na watu waliomwambia Isa habari za Wagalilaya ambao Pilato aliwaua, na damu ya hao watu akaichanganya na dhabihu yao waliyokuwa wanatoa. 2 Isa akawauliza, "Mnadhani kwamba hawa Wagalilaya ambao walikufa kifo kama hicho walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? 3 La hasha! Ninyi nanyi msipotubu, mtaangamia vivyo hivyo. 4 Au wale watu kumi na wanane waliokufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu: mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote walioishi Yerusalemu? 5 Nawaambia, la hasha! Ninyi nanyi msipotubu, wote mtaangamia vivyo hivyo."