Publicidade

Lucas 17

12 Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali, 13 wakapaza sauti, wakasema, "Isa, Bwana, tuhurumie!"

14 Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajioneshe kwa makuhani." Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika.

15 Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Isa, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. 16 Akajitupa miguuni mwa Isa akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.

17 Isa akauliza, "Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? 18 Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?" 19 Isa akamwambia, "Inuka na uende zako, imani yako imekuponya."

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-