Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 19

2 Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo. 3 Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Isa ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza, kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo. 4 Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati wa watu akapanda juu ya mkuyu ili amwone Isa, kwa sababu angeipitia njia ile.

5 Isa alipofika pale chini ya huo mkuyu, akatazama juu, akamwambia, "Zakayo, shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani mwako!" 6 Hivyo Zakayo akashuka upesi, akamkaribisha Isa nyumbani mwake kwa furaha kubwa.

7 Watu wote walipoona hivyo, wakaanza kunung’unika wakisema, "Ameenda kuwa mgeni wa mtu mwenye dhambi."

8 Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana Isa, "Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango."

Veja também