Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 19

Isa aingia Yerusalemu kwa shangwe

28 Baada ya Isa kusema haya, alitangulia kupanda kwenda Yerusalemu. 29 Naye alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima ulioitwa Mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili, akawaambia, 30 "Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtampata mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa. 31 Kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua?Mwambieni, Bwana anamhitaji.’ "

32 Wale waliotumwa wakaenda, wakapata kila kitu kama Isa alivyowaambia. 33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana-punda, wenyewe wakawauliza, "Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?"

34 Wale wanafunzi wakajibu, "Bwana anamhitaji."

35 Wakamleta kwa Isa, nao baada ya kutandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, wakampandisha Isa juu yake. 36 Alipokuwa akienda, watu wakatandaza mavazi yao barabarani.

37 Alipokaribia mahali yanapoanzia miteremko ya Mlima wa Mizeituni, umati wote wa wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa furaha kwa sauti kuu kwa ajili ya matendo yote ya miujiza waliyoyaona. Wakasema:

38 "Amebarikiwa mfalme ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!"

"Amani mbinguni na utukufu huko juu sana."

39 Baadhi ya Mafarisayo19:39 Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli. waliokuwamo miongoni mwa umati ule wa watu wakamwambia, "Mwalimu, waamuru wanafunzi wako wanyamaze."

40 Isa akawajibu, "Nawaambia ninyi, kama hawa watanyamaza, mawe yatapaza sauti."

Veja também