Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 2

Kuzaliwa kwa Isa

1 Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Rumi. 2 (Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alikuwa mtawala wa Siria.) 3 Kila mtu alienda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa.

4 Hivyo Yusufu akapanda kutoka mji wa Nasiri ulioko Galilaya kwenda Yudea, hadi Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. 5 Alienda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, aliyekuwa amemposa, na alikuwa mjamzito.

Veja também