Pular para o conteúdo
Publicidade

Luka 2:22-24

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Isa apelekwa Hekaluni

22 Ulipotimia wakati wa utakaso wake Mariamu kwa mujibu wa Torati ya Musa, basi Yusufu na Mariamu walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu 23 (kama ilivyoandikwa katika Torati ya Mwenyezi Mungu, kwamba, "Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu"), 24 na pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Torati ya Mwenyezi Mungu: "Hua wawili au makinda wawili wa njiwa".

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    22 Law 12:6-8Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo Torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, 23 Kut 13:2,12,15(kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto wa kiume aliye kifungua mimba wa mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana), 24 Law 5:11;12:8wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    22 Ulipotimia wakati wa utakaso wake Maria kwa mujibu wa Sheria ya Mose, basi Yosefu na Maria walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Bwana 23 (kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Bwana, kwamba, "Kila mtoto wa kiume kifungua mimba atawekwa wakfu kwa Bwana"), 24 na pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Sheria ya Bwana: "Hua wawili au makinda mawili ya njiwa."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.