3 Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili. 4 Yuda akaenda kwa viongozi wa makuhani na kwa maafisa wa walinzi wa Hekalu, akazungumza nao jinsi angeweza kumsaliti Isa. 5 Wakafurahi na wakakubaliana kumpa fedha. 6 Naye akakubali, akaanza kutafuta wakati uliofaa wa kumsaliti Isa kwao, ambapo hakuna umati wa watu.