33 Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walimsulubisha Isa pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume, na mwingine upande wake wa kushoto. 34 Isa akasema, "Baba23:34 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu., wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!" Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.
35 Watu wakasimama hapo wakimwangalia, nao viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, "Aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama yeye ndiye Al-Masihi wa Mungu, Mteule wake."
36 Askari nao wakaja, wakamdhihaki. Wakamletea siki ili anywe, 37 na wakamwambia, "Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe."
38 Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya:
Huyu ndiye
Mfalme wa Wayahudi.
39 Mmoja wa wale wahalifu waliosulubiwa pamoja naye akamtukana, akasema: "Wewe si ndiye Al-Masihi? Jiokoe mwenyewe na utuokoe na sisi."
40 Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akasema, "Je, wewe humwogopi Mungu, wakati uko kwenye adhabu hiyo hiyo? 41 Sisi tumehukumiwa kwa haki kwa kuwa tunapata tunayostahili kwa ajili ya matendo yetu. Lakini huyu mtu hajafanya kosa lolote."
42 Kisha akasema, "Isa, unikumbuke utakapokuja katika ufalme wako."
43 Isa akamjibu, "Amin, nakuambia, leo utakuwa pamoja nami Paradiso.23:43 Paradiso maana yake bustani nzuri; hapa ni mahali zinapoenda roho za watakatifu."