Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 5

Wanafunzi wa kwanza wa Isa

1 Siku moja Isa alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti5:1 yaani Bahari ya Galilaya, watu wengi walimsonga ili wapate kusikia neno la Mungu. 2 Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa, zikiwa zimeachwa hapo na wavuvi waliokuwa wanaosha nyavu zao. 3 Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka ufuoni. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua.

4 Alipomaliza kunena, akamwambia Simoni, "Sasa peleka mashua hadi kilindini kisha mshushe nyavu zenu mkavue samaki."

5 Simoni akamjibu, "Bwana5:5 Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita "Bwana" kwa heshima ya kawaida., tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua chochote. Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu."

6 Nao walipozishusha nyavu zao, wakavua samaki wengi sana, nyavu zao zikajaa zikaanza kukatika. 7 Wakawaashiria wavuvi wenzao kwenye ile mashua nyingine ili waje kuwasaidia. Wakaja, wakajaza mashua zote mbili samaki hata zikaanza kuzama.

8 Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia, alianguka miguuni pa Isa na kumwambia, "Bwana, ondoka kwangu. Mimi ni mtu mwenye dhambi!" 9 Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wameshangazwa sana na wingi wa samaki waliokuwa wamepata. 10 Vivyo hivyo wenzake Simoni, yaani Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walishangazwa pia.

Ndipo Isa akamwambia Simoni, "Usiogope, tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu." 11 Hivyo wakasogeza mashua zao hadi ufuoni mwa bahari, wakaacha kila kitu na kumfuata.

Veja também