12 Ikawa katika siku hizo Isa alienda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. 13 Kulipopambazuka, akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume:
14 Simoni (aliyemwita Petro) na Andrea nduguye,
Yakobo,
Yohana,
Filipo,
Bartholomayo,
15 Mathayo,
Tomaso,
Yakobo mwana wa Alfayo,
Simoni aliyeitwa Zelote6:15 Wazelote walikuwa kikundi cha Kiyahudi wenye imani kali waliompinga Kaisari na utawala wa Rumi.,
16 Yuda mwana wa Yakobo,
na Yuda Iskariote, aliyekuwa msaliti.
Isa afundisha na kuponya wagonjwa
(Mathayo 4:23-25)