Isa amponya mtu aliyepooza mkono
6 Ikawa siku nyingine ya Sabato, Isa aliingia ndani ya sinagogi6:6 Nyumba ya ibada na mafunzo. na akawa anafundisha. Huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. 7 Mafarisayo na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato. 8 Lakini Isa alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, "Inuka usimame mbele ya watu wote." Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote.
9 Ndipo Isa akawaambia wale walimu wa Torati na Mafarisayo, "Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?"
10 Akawatazama watu wote waliokuwepo, kisha akamwambia yule mtu, "Nyoosha mkono wako!" Akaunyoosha, na mkono wake ukawa umeponywa kabisa.