Pular para o conteúdo
Publicidade

Lucas 7

24 Wajumbe wa Yahya walipoondoka, Isa akaanza kusema na umati wa watu kuhusu Yahya. Akawauliza, "Mlipoenda kule nyikani, mlienda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? 25 Kama sivyo, mlienda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha! Watu wanaovaa mavazi ya kifahari na kuishi maisha ya anasa wako katika majumba ya kifalme. 26 Lakini mlienda kuona nini? Mlienda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. 27 Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa:

" Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,

atakayetengeneza njia mbele yako.

28 Nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hakuna aliye mkuu kuliko Yahya. Lakini yeye aliye mdogo kabisa katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yahya."

29 (Watu wote, hata watoza ushuru, waliposikia maneno ya Isa, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni haki, maana walikuwa wamebatizwa na Yahya. 30 Lakini Mafarisayo7:30 Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli. na wataalamu wa Torati walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokubali kubatizwa na Yahya.)

Veja também