26 Lakini mlienda kuona nini? Mlienda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. 27 Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa:
" ‘Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,
atakayetengeneza njia mbele yako.’
28 Nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hakuna aliye mkuu kuliko Yahya. Lakini yeye aliye mdogo kabisa katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yahya."