49 Isa alipokuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani mwa Yairo, yule kiongozi wa sinagogi, kumwambia, "Binti yako amekwisha kufa. Usiendelee kumsumbua Mwalimu."
50 Isa aliposikia jambo hili, akamwambia Yairo, "Usiogope. Amini tu, naye binti yako atapona."
51 Walipofika nyumbani mwa Yairo, hakumruhusu mtu yeyote aingie ndani naye isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, pamoja na baba na mama wa yule binti. 52 Wakati ule ule watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili ya huyo binti. Isa akawaambia, "Acheni kulia. Huyu binti hajafa, ila amelala."
53 Wao wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekwisha kufa. 54 Isa akamshika yule binti mkono na kuita, "Binti, amka!" 55 Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara moja. Akaamuru apewe kitu cha kula. 56 Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini Isa akawakataza wasimwambie mtu yeyote kuhusu yale yaliyotukia.