32 Petro na wenzake walikuwa wamelala usingizi mzito. Walipoamka, wakaona utukufu wa Isa na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. 33 Musa na Ilya walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Isa, "Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya." Lakini Petro hakujua alichosema.