6 " ‘Hakuna mtu yeyote atakayemsogelea ndugu wa karibu ili kukutana naye kimwili. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
7 " ‘Usimvunjie heshima baba yako kwa kukutana kimwili na mama yako. Yeye ni mama yako; usiwe na mahusiano kama hayo naye.
8 " ‘Usikutane kimwili na mke wa baba yako; hiyo itamvunjia heshima baba yako.
9 " ‘Usikutane kimwili na dada yako, wala binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo au mahali pengine.
10 " ‘Usikutane kimwili na binti ya mwanao ama binti ya binti yako; utajivunjia heshima.
11 " ‘Usikutane kimwili na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa na baba yako; huyo ni dada yako.
12 " ‘Usikutane kimwili na dada wa baba yako; ni ndugu wa karibu wa baba yako.
13 " ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako, kwa sababu ni ndugu wa mama yako wa karibu.
14 " ‘Usimvunjie heshima ndugu wa baba yako, kwa kukutana kimwili na mke wake; yeye ni shangazi yako.
15 " ‘Usikutane kimwili na mkwe wako, yeye ni mke wa mwanao; usiwe na mahusiano kama hayo naye.
16 " ‘Usikutane kimwili na mke wa kaka yako; utamvunjia heshima kaka yako.
17 " ‘Usikutane kimwili na mwanamke kisha na binti yake. Usikutane kimwili na binti ya mwanawe au binti ya binti yake; hao ni ndugu zake wa karibu. Huo ni uovu.
18 " ‘Usimchukue dada wa mke wako kuwa mke mwenza, na kukutana naye kimwili wakati bado mke wako anaishi.
19 " ‘Usimsogelee mwanamke ili kukutana naye kimwili wakati wa unajisi wa siku zake za mwezi.
20 " ‘Usikutane kimwili na mke wa jirani yako na kujitia naye unajisi.
21 " ‘Usimtoe kafara mtoto wako yeyote kwa Moleki, kwani hutalinajisi kamwe jina la Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
22 " ‘Usikutane kimwili na mwanaume vile mwanaume anavyokutana kimwili na mwanamke; hilo ni chukizo.
23 " ‘Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu.