Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 10

Isa amponya kipofu Bartimayo

46 Kisha wakafika Yeriko. Isa alipokuwa akiondoka mjini na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mmoja, jina lake Bartimayo (maana yake "mwana wa Timayo"), alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. 47 Aliposikia kuwa ni Isa Al-Nasiri aliyekuwa anapita, akaanza kupaza sauti akisema, "Isa, Mwana wa Daudi10:47 Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (Zaburi 89:3-4)., nihurumie!"

48 Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya, lakini yeye akazidi kupaza sauti, akisema, "Mwana wa Daudi, nihurumie!"

49 Isa akasimama na kusema, "Mwiteni."

Hivyo wakamwita yule mtu kipofu, wakamwambia, "Jipe moyo! Inuka, anakuita." 50 Akiwa analivua lile joho lake, alisimama na kumwendea Isa.

51 Isa akamuuliza, "Unataka nikufanyie nini?"

Yule kipofu akajibu, "Mwalimu, nataka kuona."

52 Isa akamwambia, "Nenda zako, imani yako imekuponya." Mara akapata kuona, akamfuata Isa njiani.

Veja também