22 Walimu wa Torati walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, "Amepagawa na Beelzebuli3:22 kwa Kiyunani ni Beelzebubu, yaani mkuu wa pepo wachafu! Anatoa pepo wachafu kwa nguvu ya mkuu wa pepo wachafu!"
23 Basi Isa akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: "Shetani awezaje kumtoa Shetani? 24 Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama. 25 Nayo nyumba ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama. 26 Na kama Shetani akijipinga mwenyewe na awe amegawanyika, hawezi kusimama, bali mwisho wake umetimia. 27 Hakuna mtu yeyote awezaye kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali yake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu. Ndipo ataweza kuteka nyara mali yake. 28 Amin, nawaambia, watu wataweza kusamehewa dhambi na kufuru zao zote; 29 lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele."
30 Isa alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema, "Ana pepo mchafu."