33 Akawauliza, "Mama yangu na ndugu zangu ni nani?"
34 Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, "Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. 35 Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu."