22 Kisha mmoja wa viongozi wa sinagogi5:22 Nyumba ya ibada na mafunzo. aliyeitwa Yairo akafika pale. Naye alipomwona Isa, akapiga magoti miguuni pake, 23 akamsihi akisema, "Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye ataishi." 24 Hivyo Isa akaenda pamoja naye.
Umati mkubwa wa watu wakamfuata, nao watu wakawa wanamsonga.