Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 5

25 Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na mbili. 26 Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya. 27 Alikuwa amesikia habari za Isa, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, 28 kwa maana alisema moyoni mwake, "Nikiligusa vazi lake tu, nitaponywa." 29 Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa.

30 Ghafula Isa akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akageukia umati wa watu na kuuliza, "Ni nani aliyegusa mavazi yangu?"

31 Wanafunzi wake wakamjibu, "Unaona jinsi watu wanavyokusonga. Wawezaje kuuliza, Ni nani aliyenigusa?’ "

32 Lakini Isa akaangalia pande zote ili aone ni nani aliyemgusa. 33 Yule mwanamke, akijua kilichomtokea, akaja, akaanguka miguuni pake akitetemeka kwa hofu, akamweleza ukweli wote. 34 Isa akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako."

Veja também