Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 6

22 Binti Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani.

Mfalme Herode akamwambia yule binti, "Niombe kitu chochote utakacho, nami nitakupa." 23 Tena akamwahidi kwa kiapo, akamwambia, "Chochote utakachoomba nitakupa, hata kama ni nusu ya ufalme wangu."

24 Yule binti akatoka nje, akaenda kumuuliza mama yake, "Niombe nini?"

Mama yake akamjibu, "Omba kichwa cha Yahya."

25 Yule binti akarudi haraka kwa mfalme, akamwambia, "Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yahya kwenye sinia."

26 Mfalme akasikitika sana, lakini kwa sababu alikuwa ameapa viapo mbele ya wageni wake, hakutaka kumkatalia. 27 Mara mfalme akatuma askari mmoja wa walinzi wake kukileta kichwa cha Yahya. Akaenda na kumkata Yahya kichwa humo gerezani, 28 akakileta kichwa chake kwenye sinia na kumpa yule msichana, naye yule msichana akampa mama yake.

Veja também