Pular para o conteúdo
Publicidade

Marcos 8

Isa amponya Kipofu huko Bethsaida

22 Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta mtu mmoja kipofu wakamsihi Isa amguse. 23 Isa akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Isa akamuuliza, "Unaona chochote?"

24 Yule kipofu akaangalia, akasema, "Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea."

25 Isa akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. 26 Isa akamtuma nyumbani mwake, akamwambia, "Hata kijijini usiingie."

Veja também