8 "Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.
"Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’
"Mnaniibia zaka na dhabihu. 9 Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kuwe na chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili," asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, "nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi hata mkose nafasi ya kutosha.