Publicidade

Mateus 1

Kuzaliwa kwa Isa

18 Kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu. 19 Kwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, hivyo basi alikusudia kumwacha kwa siri.

20 Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, "Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mungu. 21 Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Isa1:21 Isa ni Iesous kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua; maana yake Yehova ni wokovu., kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao."

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-