Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 1

20 Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, "Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mungu. 21 Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Isa1:21 Isa ni Iesous kwa Kiyunani, na kwa Kiebrania ni Yoshua au Yeshua; maana yake Yehova ni wokovu., kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao."

22 Haya yote yalitukia ili litimie lile Mwenyezi Mungu alilonena kupitia nabii, aliposema: 23 "Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina Imanueli" (maana yake, "Mungu pamoja nasi").

24 Yusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya jinsi alivyoagizwa na malaika wa Mwenyezi Mungu, akamchukua Mariamu kuwa mke wake. 25 Lakini hawakukutana kimwili hadi Mariamu alipojifungua mwanawe1:25 tafsiri zingine husema kifungua mimba; akamwita jina Isa.

Veja também