Publicidade

Mateus 13

Mfano wa magugu

24 Isa akawaambia mfano mwingine, akasema: "Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25 Lakini wakati kila mtu alipokuwa amelala, adui yake akaja na kupanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26 Ngano ilipoota na kutoa masuke, magugu nayo yakatokea.

27 "Watumishi wa yule mwenye shamba wakamjia na kumwambia, Bwana, si tulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Basi, magugu yametoka wapi?

28 "Akawajibu, Adui ndiye alifanya jambo hili.

"Wale watumishi wakamuuliza, Je, unataka twende tukayang’oe?

29 "Lakini akasema, Hapana, msiyang’oe, kwa maana wakati mking’oa magugu mnaweza mkang’oa na ngano pamoja nayo. 30 Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja hadi wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ "

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-