29 Isa akamwambia, "Njoo."
Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Isa. 30 Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, akapaza sauti na kusema, "Bwana, niokoe!"
31 Mara Isa akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, "Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?"