Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 15

Imani ya mwanamke Mkanaani

21 Isa aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. 22 Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, "Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi15:22 Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (Zaburi 89:3-4).! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana."

23 Lakini Isa hakumjibu neno. Hivyo wanafunzi wake wakamwendea na kumsihi sana, wakisema, "Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele."

24 Isa akajibu, "Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea."

25 Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Isa, akasema, "Bwana, nisaidie!"

26 Isa akajibu, "Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."

27 Yule mwanamke akajibu, "Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwa meza za bwana zao."

28 Ndipo Isa akamwambia, "Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka." Naye binti yake akapona tangu saa ile.

Veja também