Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 15

3 Isa akawajibu, "Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? 4 Kwa maana Mungu alisema, Waheshimu baba yako na mama yako,na, Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.5 Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,6 basi hana tena sababu ya kumheshimu baba yake nacho. Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. 7 Ninyi wanafiki! Isaya alikuwa sawa alipotabiri juu yenu kwamba:

8 " Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao,

lakini mioyo yao iko mbali nami.

9 Huniabudu bure;

nayo mafundisho yao

ni maagizo ya wanadamu tu.’ "

Veja também