Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 16

Petro amkiri Isa kuwa Al-Masihi

13 Basi Isa alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, "Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?"

14 Wakamjibu, "Baadhi husema ni Yahya; wengine husema ni Ilya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmoja wa manabii."

15 Akawauliza, "Je, ninyi mnasema mimi ni nani?"

16 Simoni Petro akamjibu, "Wewe ndiwe Al-Masihi16:16 Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta., Mwana wa Mungu aliye hai."

Veja também