Chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo
5 Wanafunzi wake walipofika ng’ambo ya bahari, walikuwa wamesahau kuchukua mikate. 6 Isa akawaambia, "Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo."
7 Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, "Ni kwa sababu hatukuleta mikate."
8 Isa, akifahamu majadiliano yao, akauliza, "Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate? 9 Je, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano kwa watu elfu tano, na idadi ya vikapu vilivyojaa mabaki mlivyokusanya? 10 Au ile mikate saba kwa watu elfu nne na idadi ya vikapu vilivyojaa mabaki mlivyokusanya? 11 Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo." 12 Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi kuhusu chachu ya kutengeneza mikate, bali kuhusu mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.