Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 17

Isa abadilika sura

1 Siku sita baada ya jambo hili, Isa akawachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake Yakobo, akawapeleka juu ya mlima mrefu peke yao. 2 Wakiwa huko, Isa alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama nuru. 3 Ghafula wakawatokea mbele yao Musa na Ilya, wakizungumza na Isa.

4 Ndipo Petro akamwambia Isa, "Bwana, ni vyema sisi tukae hapa. Ukitaka, nitafanya vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya."

5 Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililong’aa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye."

Veja também