Isa amponya kijana mwenye pepo mchafu
14 Walipofika penye umati wa watu, mtu mmoja akamjia Isa na kupiga magoti mbele yake, akasema, 15 "Bwana17:15 Wale ambao hawakumfahamu Isa kuwa Masihi walimwita "Bwana" kwa heshima ya kawaida., mhurumie mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara kwa mara huanguka kwenye moto au kwenye maji. 16 Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya."
17 Isa akajibu, "Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi hadi lini? Nitawavumilia hadi lini? Mleteni mvulana hapa kwangu." 18 Isa akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona tangu saa hiyo.