23 Ndipo Isa akawaambia wanafunzi wake, "Amin, nawaambia, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. 24 Tena nawaambia, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
25 Wanafunzi wake waliposikia haya, walishangaa sana na kuuliza, "Ni nani basi awezaye kuokoka?"
26 Lakini Isa akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu."