Ombi la mama yao Yakobo na Yohana
20 Kisha mama yao wana wa Zebedayo akamjia Isa pamoja na wanawe, naye akapiga magoti mbele yake, akamwomba Isa amfanyie jambo fulani.
21 Isa akamuuliza, "Unataka nini?" Akajibu, "Tafadhali, wajalie wanangu hawa ili mmoja aketi upande wako wa kuume, na mwingine upande wako wa kushoto katika ufalme wako."
22 Isa akawaambia, "Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe nitakachonywea mimi?"
Wakajibu, "Tunaweza."
23 Isa akawaambia, "Kwa kweli kikombe changu mtakinywea, lakini kuketi upande wangu wa kuume au wa kushoto si langu mimi kuwapa. Nafasi hizo ni za wale ambao wameandaliwa na Baba20:23 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. yangu."