Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 25

Kondoo na mbuzi

31 "Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake na malaika wote watakatifu pamoja naye, ndipo atakapoketi kwenye kiti cha enzi cha utukufu wake. 32 Mataifa yote watakusanyika mbele zake, naye atawatenga kama mchungaji anavyotenga kondoo na mbuzi. 33 Atawaweka kondoo upande wake wa kuume, na mbuzi upande wake wa kushoto.

34 "Ndipo Mfalme atawaambia wale walio upande wake wa kuume, Njooni, ninyi mliobarikiwa na Baba25:34 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. yangu; urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 35 Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha, 36 nilikuwa uchi mkanivisha nguo, nilikuwa mgonjwa mkanitunza, nami nilikuwa kifungoni mkaja kunitembelea.

37 "Ndipo wale wenye haki watakapomjibu, Bwana, ni lini tulikuona ukiwa na njaa tukakulisha, au ukiwa na kiu tukakunywesha? 38 Lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha, au ukiwa uchi tukakuvisha nguo? 39 Tena ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa tukakutunza, au ukiwa kifungoni tukakutembelea?

40 "Naye Mfalme atawajibu, Amin nawaambia, kwa jinsi mlivyomtendea mmoja wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

41 "Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika wake. 42 Kwa maana nilikuwa na njaa nanyi hamkunipa chakula, nilikuwa na kiu nanyi hamkuninywesha, 43 nilikuwa mgeni nanyi hamkunikaribisha, nilikuwa uchi nanyi hamkunivisha nguo, nilikuwa mgonjwa nanyi hamkunitunza, na nilikuwa gerezani nanyi hamkuja kunitembelea.

44 "Ndipo wao pia watajibu, Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au uchi, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?

45 "Naye atawajibu, Amin nawaambia, kwa jinsi hamkumtendea mmoja wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkunitendea mimi.

46 "Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também