Yahya atayarisha njia
1 Siku hizo Yahya alikuja akihubiri katika nyika ya Yudea, akisema, 2 "Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia." 3 Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema:
"Sauti ya mtu aliaye nyikani,
‘Itengenezeni njia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,
yanyoosheni mapito yake.’ "
4 Basi Yahya alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5 Watu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Yudea yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani. 6 Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza3:6 Ubatizo ni ishara ya kuungama dhambi na kusamehewa na Mwenyezi Mungu, na kuweka nadhiri ya kubadilisha mienendo ya awali. katika Mto Yordani.