Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 3:11,13-17

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

11 "Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu wa Mungu3:11 au katika Roho wa Mungu na kwa moto.

13 Kisha Isa akaja kutoka Galilaya hadi Mto Yordani ili Yahya ambatize. 14 Lakini Yahya akajitahidi kumzuia, akimwambia, "Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?"

15 Lakini Isa akamjibu, "Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote." Hivyo Yahya akakubali.

16 Naye Isa alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. 17 Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa; ninapendezwa sana naye."

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    11 Yn 1:15,26,27,33;Mdo 1:5Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

    13 Mk 1:9-11;Lk 3:21-22;Yn 1:31-34Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? 15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Ndipo akakubali. 16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, na kutua juu yake; 17 Mwa 22:2;Zab 2:7;Isa 42:1;Mt 12:18;17:5;Mk 1:11;Lk 9:35na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    11 "Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu3:11 …kwa Roho Mtakatifu hapa ina maana ya katika Roho Mtakatifu. na kwa moto.

    13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Mto Yordani ili Yohana ambatize. 14 Lakini Yohana akajitahidi kumzuia, akimwambia, "Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?"

    15 Lakini Yesu akamjibu, "Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote." Hivyo Yohana akakubali.

    16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. 17 Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.