13 Kisha Isa akaja kutoka Galilaya hadi Mto Yordani ili Yahya ambatize. 14 Lakini Yahya akajitahidi kumzuia, akimwambia, "Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?"
15 Lakini Isa akamjibu, "Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote." Hivyo Yahya akakubali.