Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 3:7-10

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

7 Lakini alipowaona Mafarisayo3:7 Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli. na Masadukayo3:7 Kundi la kidini la Wayahudi; waliamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho. wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: "Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 8 Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. 9 Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka kwa mawe haya. 10 Hata sasa shoka limeshawekwa tayari katika shina la kila mti, basi kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    7 Mt 12:34;23:33;Mwa 3:15Na alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazawa wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 8 Basi zaeni matunda yapasayo toba; 9 Yn 8:33,39;Rum 2:28,29;4:12wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto. 10 Mt 7:19;Lk 13:6-9;Yn 15:6Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    7 Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: "Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? 8 Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. 9 Wala msidhani mnaweza kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Abrahamu, baba yetu.’ Nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka kwa mawe haya. 10 Hata sasa shoka limeshawekwa tayari kwenye shina la kila mti, basi kila mti usiozaa matunda mazuri, hukatwa na kutupwa motoni.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.