Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 4

Isa ajaribiwa nyikani

1 Kisha Isa akaongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu hadi nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. 2 Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. 3 Mjaribu akamjia na kumwambia, "Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu4:3 Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1), wa kiroho, bali si wa kimwili., amuru mawe haya yawe mikate."

4 Lakini Isa akajibu, "Imeandikwa: Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ "

5 Ndipo ibilisi akampeleka Isa hadi mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu4:5 Nyumba kuu ya ibada kwa Waisraeli iliyokuwa Yerusalemu., 6 akamwambia, "Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa:

" Atakuagizia malaika wake,

nao watakuchukua mikononi mwao

ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ "

7 Isa akamjibu, "Pia imeandikwa: Usimjaribu Mwenyezi Mungu, Mungu wako.’ "

8 Kwa mara nyingine, ibilisi akampeleka Isa hadi kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonesha falme zote za dunia na fahari zake, 9 kisha akamwambia, "Nitakupa hivi vyote ukinisujudia na kuniabudu."

10 Isa akamwambia, "Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, Mwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ "

11 Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.

Veja também