Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 4

Wanafunzi wa kwanza wa Isa

18 Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa walikuwa wavuvi. 19 Isa akawaambia, "Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu." 20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

21 Alipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Isa akawaita. 22 Nao mara moja wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata.

Veja também