16 Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. 17 Haya yalifanyika ili litimie neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya, kwamba:
"Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu
na akachukua magonjwa yetu."