Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 8

Isa atuliza dhoruba

23 Naye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata. 24 Ghafula, kukatokea dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Isa alikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, "Bwana, tuokoe! Tunazama!"

26 Naye Isa akawaambia, "Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?" Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nayo bahari ikatulia kabisa.

27 Wale watu wakashangaa, wakisema, "Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!"

Veja também