Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 8

Watu wawili wenye pepo wachafu waponywa

28 Walipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile. 29 Wakapaza sauti wakisema, "Una nini nasi, Mwana wa Mungu8:29 Yaani Mwana wa asili moja na Mwenyezi Mungu (Yohana 1:1-2), wa kiroho, bali si wa kimwili.? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati ulioamriwa?"

30 Mbali kidogo kutoka pale walipokuwa, kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakila. 31 Wale pepo wachafu wakamsihi Isa, "Ukitutoa humu, turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe."

32 Akawaambia, "Nendeni!" Hivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremka gengeni kwa kasi, likaingia katika ziwa na kufa ndani ya maji. 33 Wale watu waliokuwa wakiwachunga hao nguruwe wakakimbia wakaingia mjini, wakaeleza yote yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu. 34 Kisha watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Isa. Nao walipomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.

Veja também