Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 9

Isa awaponya Vipofu

27 Isa alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti na kusema, "Mwana wa Daudi9:27 Ina maana kwamba Isa ni mrithi wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu (Zaburi 89:3-4)., tuhurumie!"

28 Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Isa akawauliza, "Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?"

Wakamjibu, "Ndiyo, Bwana."

29 Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, "Iwe kwenu sawasawa na imani yenu." 30 Macho yao yakafunguka. Isa akawaonya vikali, akisema, "Chungeni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili." 31 Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.

Veja também