4 Mfalme akaniambia, "Je, haja yako ni nini?"
Ndipo nikaomba kwa Mungu wa mbinguni, 5 na nikamjibu mfalme, "Ikimpendeza mfalme, na kama mtumishi wako amepata kibali machoni pake, anitume kule mji wa Yuda, mahali baba zangu walipozikwa, ili niweze kuujenga upya."